VIJANA IMARA

VIJANA IMARA

Programu ya Vijana Imara inalenga kuwawezesha watoto na vijana katika hatua mbalimbali za maisha yao kujenga uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda kwa misingi ya maadili. Programu hii inajikita katika kukuza uelewa wa kina juu ya mchango wa maadili katika elimu, mahusiano, ajira, uchumi na maendeleo binafsi. Kupitia elimu ya maadili, mijadala ya hoja, ushauri nasaha na matumizi ya majukwaa ya kisasa ya mawasiliano (vyomo vya habari na mitandao ya kijamii), programu inalenga kuandaa kizazi chenye nidhamu, uwajibikaji na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata bila shinikizo la adhabu au matarajio ya zawadi.

Makundi yanayolengwa:

  • Watoto chini ya Wazazi/Walezi na viongozi wa dini
  • Vijana mashuleni (msingi, sekondari, elimu ya juu)
  • Vijana wanaoanza familia (ndoa, uzazi)

Lengo:

  • Kujenga  vijana wenye uwezo wa kufikiri kimaadili, si kufuata mkumbo bila hoja ya msingi
  • Kutoa elimu jinsi maadili yanavyoathiriwa na kuathiri elimu, mahusiano, kazi na uchumi, mafanikio na hivyo kuona maadili kama kitovu cha mafanikio na si kikwazo cha mafanikio
  • Kujenga vijana wenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na wapo tayari kuwajibikaji
  • Kujenga vijana wenye uzalendo na hali ya kujituma kwa maslahi mapana ya Taifa