MAZINGIRA IMARA

MAZINGIRA IMARA

Programu ya Mazingira Imara inalenga kukuza maadili ya uwajibikaji katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai. Inahusisha kukuza uelewa juu ya haki za wanyama, uhifadhi wa rasilimali na uelewa wa athari za mmomonyoko wa maadili kwa mazingira. Programu inalenga kuonyesha kuwa uharibifu wa mazingira ni matokeo ya kushuka kwa maadili, na kwamba kulinda mazingira ni wajibu wa kimaadili kwa binadamu na vizazi vijavyo.

Vipengele yanayolengwa:

  • Vijana na watoto
  • Walimu na wasimamizi wa watoto
  • Wawindaji na wasaidizi wa watalii
  • Wafugaji na wakulima
  • Viongozi wa dini, siasa na mila na makundi ya kijamii
  • Madereva wa vyombo vya moto na usafiri wa umma na abiria
  • Wajenzi wa Wachimbaji wa madini
  • Wamiliki wa viwanda na wawekezaji

Lengo:

  • Kukuza uelewa wa kimaadili kuhusu utunzaji wa mazingira na rasilimali
  • Kujenga hali ya kuthamini viumbe hai kwa kuelimisha jamii juu ya haki za wanyama na wajibu wa binadamu katika kuwalinda.
  • Kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na mmomonyoko wa maadiliKuwajengea vijana uwezo wa kufanya maamuzi ya kimaadili yanayolinda mazingira kwa masrahi ya kizazi cha sasa na kijacho
  • Kushirikisha viongozi wa dini, mila, siasa na jamii katika kusimamia na kuimarisha maadili ya mazingira kwa uwajibikaji wa pamoja.
  • Kukuza uwiano kati ya maendeleo ya kiuchumi na ulinzi wa mazingira kwa kuhamasisha uwekezaji na shughuli za kiuchumi zenye maadili na uendelevu.
  • Kuchochea tafiti na mijadala ya kitaaluma kuhusu uhusiano kati ya maadili na mazingira ili kuongoza sera, elimu na vitendo vinavyolinda mazingira