Haki za Wanyama: Kipimo kilichosahaulika cha maadili ya jamii
Katika jamii nyingi za Tanzania, mfano wa jamii karibu zote Frika, haki za wanyama ni mjadala usiopewa uzito. Wengi hufumbia macho, si kwa sababu ni waovu, bali kwa sababu hawajawahi kufundishwa kuunganisha mateso ya wanyama na tabia za binadamu. Tumezoea kuona mnyama kama kitu cha kutumia, si kiumbe chenye hisia. Tatizo ni kubwa kuliko wengi tunavyofikiri, hibi umwewahi kufikia kuwa 'jamii inayodharau maumivu ya viumbe wasioongea, hujenga kizazi kinachoamini kuwa kutokuwa na sauti ni sawa na kutokuwa na haki.
Kimya Sio Ishara ya Kutokuhisi Maumivu
Mnyama haongei kwa lugha yetu, lakini anaumia. Anaogopa. Anakimbia maumivu. Anapigania uhai wake. Ukimkanyaga mkia, anapiga kelele. Ukimnyima chakula, anadhoofika. Ukimtesa, anateseka kimya kimya.
Tatizo si kwamba wanyama hawaumii, ni kwa vile tu, tumefundishwa kuwa kama unaweza kapambana na kujitetea basi utaheshimika, na kama hauweiz kujieleza aua kulipiza basi utaonewa kwakuwa hakuna nayejua maumivu yako.
Bila shaka kauli hizi si ngeni kuzisikia mtaani. 'wacha nimpige tu huyu pakaa kwani anaumia?', 'sitampa chakula leo kwana atanisemea?', 'yeye si mnyama tu atavumilia', 'amekonda kama mbwa', 'amaepigwa kipigo cha mbwa', 'amaefnyiwa ukatili wa kinyama'au 'amauwawa kama myama'. Kwakuwa maneno haya tumekuwa huku tukiyaskia tunaweza dhani ni ya kawaida lakini tunashindwa kufahama nguvu kubwa ya kueneza utakitili iliyobebwa ndani yake. Hapo ndipo mzizi wa ukatili unapoanzia, leo kijana atamfanyia mnyama unapuuzia kwakuwa mnyama haongei kujieleza kwamba anaumia, kesho kijana akishakuwa na roho ngumu atamndea ukatili huo binti mnyonge asiye na sauti mbele ya jamii ambaye hawezi kupaza zauti na kupewa nafasi ya kusikilizwa na badae siku binti huyu akiweza kusikilizwa na kueleza magumu anayopitia ndipo tutamuhukumu kijana huyu kwamba amefanyia ukatili kama vile mnanyama, hii ni kwa kwa sababu tulitegemea mnyama ndiye anastahili kufanyiwa ukatili. Mwanafalsafa maarufu, Arthur Schopenhauer anasema "Kama wanyama wangeweza kusema mateso yao, basi wangetikisa maadili na ustaarabu wetu".
Tanzania na Maisha ya Kila Siku ya Wanyama
Katika mazingira yetu, wanyama wako karibu sana na maisha ya binadamu. Wanatumika kulima, kubeba mizigo, kulisha familia, wanatumika kuzalisha na kutengenezwa kama bidhaa, wanatumika kama chakula, kuendesha mila na hata kufanya tafiti mbali mbali. Tatizo halianzii hapo. Tatizo linaanza pale matumizi yanapogeuka kuwa mateso yasiyo na sababu kwani imekuwa kawaida kuona wanyama:
- Wakipigwa kupita kiasi ili afanye kazi,
- Wakitembea na majeraha bila kutibiwa,
- Wakichomwa moto kuwekewa 'urembo na arama',
- Wakichinjwa mbele ya wenzake na
- Wakichunwa akiwa bado hai.
Yote haya hufanyika hadharani, mbele ya watoto, kana kwamba ni jambo la kawaida. Lakini kimaadili, hakuna jambo la kawaida katika mateso yasiyo ya lazima.
Tunachowafundisha Watoto Bila Kujua
Mtoto anapokua akiona mnyama anateswa, anajifunza somo bila kuambiwa neno kwamba:
- Mwenye nguvu ana haki ya kufanya chochote kwa yule asiyeweza kujitetea,
- Ni haki mnyonge kuumizwa kwakuwa hakuna wa kumsaidia na hawezi kujilipia, na
- Hat binadamu wasioweza kujieleza kama walemavu wa akili, bubu kizwi, watoto wado, wagonjwa na wasiojua lugha ya wenyeji wanafaa kutendewa ukatili kwani hawawezi kusema maumivu yao na kusikilizwa na yeyote.
Mtoto huyo akikua, si ajabu akiwa katili kwani atakuwa zao la mfumo unao fanya ukatili kwa wanyama kwa dhana ya kwamba hawawezi kuongea na hivyo hawasikii maumivu. Hapo ndipo jamii inapoanza kuzalisha watu wakatili kwa vitendo, lakini wanafiki kwa maneno, wanaozungumzia haki za binadamu huku wakifurahia mateso ya viumbe dhaifu.
Maadili ya Kweli Huanza Pale Unapotenga wema bila kusukumwa na uoga
Ni rahisi kuwa “mtu mzuri” mbele ya mwenye mamlaka. Ni rahisi kutenda haki kwa anayekuona na anaweza kukuripoti. Lakini maadili ya kweli huonekana unapokuwa na uwezo wa kudhulumu bila adhabu, halafu ukaamua kutodhulumu. Ni wazi kwamba Mnyama au ndege hawezi kukushitaki, kukuonea, wala kukulipiza kwa matendo yako. Ukichagua kumtendea haki, basi unafanya hivyo kwa sababu ya dhamiri safi na uadilifu, si hofu.
Na huo ndio msingi wa maadili ya kweli.
Sio Kuacha Mila, Bali Kuziweka Kwenye Utu
Kwakuwa harakati ya kupiga ukatili kwa wanyama ni changa hapa nchini, si rahisi ajenda hii kueleweka na kupokelewa mara moja, kwani watu wengi wamefanya tabia hizi kuwa maisha yao ya kila siku kwa vizizi vingi. Natambua kuwa ni ngumu na inahitaji muda, jamii kupokea ajenda hizi za mapinduzi ya kimtazamo juu ya namna tunavyoweza kuisha na viumbe hai kwa upendo bila kutazamaia faida ya moja kwa moja kutoka kwao. Hivyo Blogu hii haisemi tuache kutumia wanyama. Inasema tutumie kwa utu, na kutokea hapo utakuwa mwanzo mzuri wa kujenga hisia kati ya watu na wanyama:
- Kama ni chakula—chinja kwa staha,
- Kama ni kazi—usimzidishe,
- Kama ni tiba au mila—usimtesa bila sababu na
- Kutomchinja mbele ya wenzake si ustaarabu wa kisasa—ni maadili ya msingi.
Hitimisho: Jamii Inayoheshimu Wanyama Hulinda Binadamu Wake
Jamii inayofundisha watu wake kuheshimu viumbe wasio na sauti, hujenga msingi wa kuheshimu pia binadamu waliodhoofika—wagonjwa, wazee, watoto, maskini na waliotengwa. Lakini jamii inayocheka maumivu ya mnyama, siku moja itacheka pia maumivu ya binadamu aliyepoteza sauti yake.
Haki za wanyama ni; Ni kioo cha maadili yetu, ni darasa la huruma na pia ni mwanzo wa kujenga jamii yenye utu.